Duration 3:26

JESHI LA POLISI LINDI LATOA UFAFANUZI KUONDOA UTATA KUTEKWA KWA KATIBU WA CHADEMA.

98 watched
0
0
Published 25 Aug 2020

Jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi limekanusha taarifa zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Katibu wa CHADEMA wa wilaya ya Ruangwa, Bw. Claudio Teodori Chilemba ametekwa. Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ofisi ya Mkuu wa Polisi wa wilaya ya Ruangwa leo Agosti 24, 2020, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Lindi, Stanley Kulyamo amesema hakuna taarifa zozote za utekaji nyara kwa mtu huyo. “Agosti 8, 2020 tulikuwa na taarifa za kutoweka na kwenda kusikojulikana kwa Katibu huyo ingawa hapo awali alimuaga Mwenyekiti wake kuwa anakwenda nyumbani kwake ila hakufanya hivyo. Jeshi la Polisi lilianza kufanya uchunguzi kuhusu kutoonekana kwa Katibu huyo, Jeshi la Polisi kupitia kwa vyanzo vyake likagundua kuwa mtu huyo yupo wilayani Masasi Mkoa wa Mtwara.

Category

Show more

Comments - 0