Duration 2:42

MAABARA YA BIL.9 YAJENGWA KILIMANJARO TANGU AINGIE MAGUFULI ZIMEFIKA HOSPITALI 67

9 526 watched
0
106
Published 22 Jun 2020

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imejenga Maabara ya Kisasa ya uchunguzi wa magonjwa ya binadamu ya kuambukiza yenye thamani ya shilingi Bilion tisa katika Wilaya ya Siha Mkoani Kilimanjaro. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Maabara hiyo ikiwa inaelekea kukamilika ili kuanza kutoa huduma za uchunguzi wa magonjwa ya kuambukiza. "Mmekuwa mkisikia mara nyingi nikisema kwamba tunajenga maabara ya kisasa yenye thamani ya shilingi Bilion tisa kwenye Wilaya ya Siha, lakini leo tunaliona jengo hilo lenye thamani hiyo" alisema. Aliendelea kusema kuwa, tangia Uhuru wa nchi yetu mpaka 2015, Serikali ilikuwa na Hospitali za Wilaya sabini na saba tu, huku akiweka wazi kuwa tangia Serikali inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli iingie madarakani tayari Hospitali za Wilaya 67 zimekwisha jengwa ili kuboresha upatikanaji wa huduma za Afya. "Toka Uhuru tumekuwa na Hospitali za Wilaya sabini na saba, lakini kwa miaka hii mitano Hospitali zilizokwisha jengwa ni sitini na saba na kwenye bajeti hii, mpaka 2021 zitaenda kuwa karibia 90, maana yake tukienda kwa kasi hii huduma za Afya zitakuwa nzuri sana" alisema.

Category

Show more

Comments - 16