Duration 8:6

WAZIRI MKUU AWAKA, ALICHOKIKUTA HOSPITALI HAKIVUMILIKI, NA PESA ZIMEKWISHA

101 498 watched
0
352
Published 6 Oct 2019

WAZIRI MKUU AWAKA, ALICHOKIKUTA HOSPITALI HAKIVUMILIKI, NA PESA ZIMEKWISHA! WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hajaridhishwa na ujenzi wa kituo cha afya cha Ndago, wilayani Iramba mkoani Singida kwa sababu uko chini ya kiwango. Ametoa kauli hiyo leo (Jumapili, Oktoba 6, 2019), wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Ndago mara baada ya kukagua majengo ya kituo hicho. “Nimepita kote nchini kukagua vituo hivi lakini hapa wamenikasirisha. Wamenileta kwenye jengo nilikaguem nikajua ni jipya kumbe ni la zamani. Lazima nikiri kwamba fedha yetu hapa haijakamilika, jengo la mama na mtoto halijakamilika. Nilipouliza linakamilika lini, wananijibu tuko kwenye final touches (tuko hatua za mwisho),” amesema. “Jengo lile halivutii kabisa, wanaotoa maelezo hakuna kinachoeleweka. Sijaridhishwa kabisa na hali hii. Jengo la upasuaji nalo pia nimeona ni la zamani. Hii ina maana hamjajenga jengo jipya. Mimi nataka nione jengo jipya hapa,” amesisitiza. YALIYOMO GLOBAL TV ONLINE (+255 657 955825 au +255 784 888982) --------------------------------------------------------------------------------------- HABARI MPYA DAILY: /playlist?list ... HISTORIA ZA VIONGOZI ZA KUSISIMUA: /playlist?list ... GLOBAL RADIO TV: /playlist?list ... EXCLUSIVE INTERVIEWS: /playlist?list ...

Category

Show more

Comments - 154